Jarida la Forbes ambalo mara nyingi limekua likitoa ripoti za matajiri wa dunia na utajiri wao limesema tajiri wa Tanzania Said salim Bakhresa ambae ameshika namba 30 kati ya matajiri 40 wa Afrika aliacha shule akiwa na umri wa miaka 14 na kuanza kuuza potato mix baada ya hapo akafungua restaurant ndogo lakini leo ameajiri zaidi ya watu elfu mbili kwenye kampuni yake.
Kampuni hii ambayo inaingiza zaidi ya dola za kimarekani milioni 800 kwa mwaka na ndio kampuni inayoongoza kwa kutengeneza unga wa ngano Afrika Mashariki na kati ambapo kwa siku inatoa tani 3,200.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !