Headlines News :

Home » , » kAULI ZA WASANII MBALIMBALI WA BONGO WAKIONGELEA KIFO CHA SHARO MILIONEA

kAULI ZA WASANII MBALIMBALI WA BONGO WAKIONGELEA KIFO CHA SHARO MILIONEA

Written By Unknown on Wednesday 28 November 2012 | 02:50

MASTAA mbalimbali Bongo wameeleza masikitiko yao kufuatia kifo cha ajali ya agari cha aliyekuwa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Sharo Milionea.

 
Marehemu Hussein Mkieti 'SHARO MILIONEA' enzi za uhai wake.
Wengi wa wasanii waliozungumza na gazeti hili usiku wa saa 3 jana na kuendelea walionesha majonzi makubwa kufuatia kifo cha Sharo Milionea huku baadhi yao wakitoa sauti zenye kuashiria simanzi kubwa.
SIMON MWAKIFAMBA:
Ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Filamu Bongo (TAFF), yeye alisema Tanzania kwa mara nyingine imempoteza msanii mwenye kipaji na aliyependwa na wengi.
“Kwa kweli nimeumia sana. Sijui ni nini, Sharo Milionea ameondoka bado anapendwa na kipaji chake kilikuwa kinazidi kukua siku hadi siku. Inasikitisha sana,” alisema Mwakifamba.
 
JACQUELINE WOLPER:
Ni msanii wa filamu za Bongo. Baada ya kusikia Sharo Milionea ameaga dunia kwa ajali ya gari alidondosha machozi akisema:
“Jamani kuna nini kwetu mastaa? Sharo Milionea huyuhuyu ‘kamata mwizi men’ au kuna mwingine? Nawapa pole ndugu wote, Mungu atakuwa nao katika kipindi hiki kigumu kwao,” alisema Wolper.
MRISHO MPOTO:
Ni mwanamuziki wa nyimbo za mashairi ya kiasili. Alisema alisikia habari za kifo cha Sharo Milionea baada ya kutoka kwenye kipindi kimoja cha TBC1 jana usiku.
Anasema alishtuka sana kwani hakutegemea kijana mdogo kama Sharo angeaga dunia katika kipindi ambacho Wabongo bado wanamhitaji, lakini akasema kwa binadamu wanatakiwa kujua njia ni moja na ili mtu aende peponi lazima afe kwanza.
“Nimesikitika sana. Sharo Milionea ameondoka katika umri wa kutegemewa na taifa na familia yake pia. Nasikia alikuwa anakwenda kumsalimia mama yake mzazi kule Muheza, Tanga, lazima alimbebea zawadi mbalimbali.
“Lakini binadamu tutambue kwamba ili tufike peponi lazima tufe na kila mtu ana siku yake, ingawa ni siri ya Mwenyezi Mungu,” alisema Mpoto.
 
MICHAEL SANGU ‘MIKE’:
Ni msanii wa filamu aliyesikitishwa sana na kifo cha Sharo Milionea. Aliongea na gazeti hili jana saa 6: 05 usiku ambapo alisema hakuamini kama kweli msanii huyo aliaga dunia mpaka alipopata uthibitisho kutoka kwa vyanzo vyake vya kuaminika.
DIAMOND:
Jina lake kamili ni Nasibu Abdul, ni msanii wa Bongo Fleva ‘zao’ moja na marehemu Sharo Milionea. Yeye alipozungumza na Uwazi jana saa 5:24 usiku alionesha dalili zote za kutoamini tukio hilo.
“Ee bwana ee, mi siamini kabisa. Yaani sijui niseme nini, siwezi kusema pole wala Mungu ailaze roho yake peponi maana siamini yaani, da!” alisema mwanamuziki huyo.
 
FRED MARIKI ‘MKOLONI’:
Ni mwanamuziki wa siku nyingi kwenye gemu akiwa na Kundi la Wagosi wa Kaya kutoka Tanga. Yeye alizungumza na gazeti hili jana saa 3:12 usiku.
Alisema kifo cha Sharo Milionea ni pengo kwa sehemu kubwa kwani mbali na kuimba Bongo Fleva, pia alikuwa msanii wa kuchekesha aliyetokea kupendwa na wengi Tanzania.
“Kwa kweli Sharo Milionea naweza kusema ameacha pengo kubwa sana, maana alikuwa anaimba Bongo Fleva lakini pia alikuwa anachekesha sana. Mi binafsi nimeumia sana,” alisema mwanamuziki huyo.
Mzee Majuto (kushoto) akiwa na marehemu Sharo Milionea enzi za uhai wake.

MZEE MAJUTO:
Ni msanii wa vichekesho Bongo, pia alikuwa akifanya kazi na marehemu Sharo Milionea. Yeye aliposikia habari hizo alisema: “Naomba sana habari hizi zisiwe na ukweli wowote ule maana naweza nikaanguka. Sharo alikuwa kiungo muhimu sana kwenye kazi zangu.”
 
STEVE NYERERE:
Alisema: “Nashindwa hata kusema, naona mitihani inatuandama, Sharo alikuwa kijana na tulikuwa tunamtegemea kwamba angeendelea kufanya mambo makubwa katika sanaa yetu.”
RASHID NASORO:
Muigizaji huyo wa Kundi la Bongo Dar es Salaam, alipopata taarifa kwa mara ya kwanza alikuwa mkali, akaandika kwenye akaunti yake ya meseji za Blackberry (BBM): “Acheni uchuro, Sharo hajafa.”
Baada ya dakika tano, akaandika: “Jamani ni kweli, ndugu yetu Sharo hatunaye.”
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

 
Designed and Bloggerized by | Tryphone Chasama Jr | 0719 625003/0765860437
Proudly powered by BONGO BLOG DESIGNERS
Copyright © 2012. HABARI BONGO - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template