Sakata la mwigizaji wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel (pichani) kuvaa
nusu utupu na kukaa kihasara huku maungo nyeti yakichungulia, limechukua
sura mpya baada ya Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kumjia juu, Ijumaa
Wikienda linafunguka.
Kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa Basata, Ghonche Materego, wasanii
wamekuwa wakionywa mara kwa mara kuhusu kuzingatia maadili na kuacha
kuvaa nguo za nusu uchi hivyo inapotokea mmoja wao akawa kichwa ngumu,
basi huyo atakuwa na ugonjwa akilini hivyo anahitaji ushauri wa
kisaikolojia.
“Huyo Aunt Ezekiel anahitaji ushauri nasaha kama ambavyo tumekuwa
tukifanya kwa watu wengine wenye tatizo kama lake. Anapaswa kusikiliza
maelekezo ya Basata kwamba nguo zisizo na maadili ya Mtanzania
hazitakiwi katika sanaa yetu, aache mara moja.
“Kila Jumatatu huwa tuna Jukwaa la Sanaa hivyo tumeshakutana na wasanii
hao na kuwaeleza tatizo hilo lakini wamekuwa wagumu wa kuelewa. Tumeona
njia pekee ya kuwasaidia ni kuwapa ushauri wa bure juu ya madhara ya
kuvaa nguo hizo,” alisema mkurugenzi huyo kwa staili ya kumpa onyo kali
msanii huyo.
Hivi karibuni, Aunt akiwa kwenye ziara ya Tamasha la Serengeti Fiesta
2012 mkoani Mwanza alijikuta akilewa na kushindwa kujisitiri kutokana na
kigauni alichokuwa amevaa kilichoacha wazi sehemu kubwa ya maumbile
yake muhimu.
Home »
bongofleva
,
mchanganyiko
,
mpya
» BASATA Wamjia Juu Aunt Ezekiel Baada ya Kumwaga Radhi Mwanza
BASATA Wamjia Juu Aunt Ezekiel Baada ya Kumwaga Radhi Mwanza
Written By Unknown on Tuesday, 20 November 2012 | 04:01
Labels:
bongofleva,
mchanganyiko,
mpya
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !