Headlines News :

Home » , » Walaka wa kusikitisha kwa balozi Kagasheki wasambazwa Bukoba mjini

Walaka wa kusikitisha kwa balozi Kagasheki wasambazwa Bukoba mjini

Written By Unknown on Thursday 29 November 2012 | 02:30

Nakumbuka maneno ya MOHANDAS KARAMACHAND GANDHI aliyefahamika sana kama MAHATIMA GANDHI na baba wa taifa la India, Yeye alisema “SIWEZI KUHUBIRI AU KUPIGIA DEBE HARAKATI ZINAZOHATARISHA UVUNJIFU WA AMANI KWASABABU SI MUHUMINI WAKE, NINACHOWEZA KUHUBIRI NA KUKIPIGIA DEBE NI KUTOKUBALI KUMTII YEYOTE YULE ANAYEHATARISHA MAISHA YAKO”

Hali inayoonekana Bukoba ni suala la utekelezaji wa miradi ya jamii ambayo ipo kisheria lakini wapo wanaotaka kuitumia kama daraja la kujitangaza, katika njia ya kuwaumiza wananchi kwasababu uwezi kufanya mjadala usio na ugomvi kama upande mmoja hauna uhakika au hauelewi kinachoendelea. Sasa je wana wa Bukoba wanajua nini kuhusu mikataba ya soko na mtu akihoji katika hilo amekosea?

Kutokana na sintofahamu hiyo, wapo waliopewa idhini na wananchi kuhoji kwa niaba yao, sasa wanapohoji waliopembeni na ambao hawajui lakini wanataka kutumia daraja hilo kupata uongozi, tayari wanahubiri na kupigia debe harakati zinazohatarisha uvunjifu wa amani kwasababu wanajaza maneno kwa wasiojua mikataba ya soko iko je.

Inawezekana wakasema mengi kutokana na hisia, lakini hii inanipa picha kwamba wasemao wanaweza kuamsha wasiyoyajua au kuyafanyia kazi, ila kwasababu wanataka nafasi watayafanya makubwa ili kutimiza maandiko ya wahenga kwamba “FAHARI WAWILI WAGOMBANAPO, NYASI NDIZO ZINAUMIA”.

Mbunge akisimama katika mikutao ya adhara anazungumzia siasa na maenedeleo, mwalimu akiwa darasani anazungumzia masomo na taaluma husika kulingana na kipindi.

Kagasheki kusema amemchonga Meya, kwa mtu mwenye uelewa na akili timamu atajua amemaanisha nini lakini asiyejua chochote atajua amemaanisha sura, lakini kagasheki angekuwa mwalimu, mimi ningeelewa kuwa amemchonga meya kwakumfundisha somo Fulani ambalo limemfikisha alipo.

Hivyo basi kwakuwa ni mwanasiasa Napata picha ya moja kwa moja kwamba amemchonga kisiasa yaani amempa mwanga na mbinu za kusimama mbele ya adhara na kuzungumza kwa kujibu hoja na jinsi gani anaweza kutetea wananchi na hilo halina ubishi jamani waliokuwa bukoba tangu mapema wanalijua, sasa utasemaje MUNGU AKAMUUMBA MTU KWA MFANO WAKE? Tusidanganye wananchi.

Baba wa taifa na aliyeongoza mapinduzi ya taifa la China MAO TSE-TUNG akiongoza chama cha kikomunisti kuanzia mwaka 1935, alisema kuwa “MATABAKA UPAMBANA BAADHI HUSHINDA MAPAMBANO NLAKINI MENGINE HUSHINDWA, NA HIVYO KUTOKOMEZWA NA NDIVYO HISTORIA YA USTAARABU ILIVYO DUNIANI”.

Sasa wanaochochea hasira na chuki kwa wananchi wakitumia nafasi ya wananchi kutokuwa na makini au nafasi ya kusoma na kuelewa mambo, wajue kwamba wanayoyakuza siku moja yatafutika kwasababu historia inaonesha hivyo tangu karne zilizotangulia labda kama itakuwa mara ya kwanza kushindikana, na inaonekana yakisha malizika waliokuwa upande Fulani ulazimika kujipendekeza upande wa pili ili wapate nafasi.

Nawasihi kukumbuka maneno ya COMFUCIUS aliyezaliwa mwaka 551 BC na kufariki 497 bc, alisema kuwa “FARAJA YETU KUBWA KATIKA MAISHA NI SI KWAMBA BINADAMU KAMWE HATUANGUKI, BALI KILA TUANGUKAPO TUNAUWEZO WA KUAMKA NA KUENDELEA NA SAFARI”, hivyo pamoja na mbunge kuwa ni nafasi mojawapo ya ajira yake katika serikali ya jamhuri, bado anasemea wananchi kupitia matukio anayoyashuhudia ambayo hata hivyo hayako sawa katika maslahi ya mwananchi, kwahiyo wananchi walitaka azungumzie chumbani ili muendelee kulishwa maneno ya uongo?

Kutokana na watu kuhitaji uongozi wa lazima, wanajitokeza wanaoibua habari za uchochezi na kama tunavyotambua masuala ya UDINI hayana nafasi kwa watanzania, kitendo cha mbunge kutoa usafiri kwa shughuli mbalimbali kimekuwa kikifanyika tangu mbunge huyu amechukuwa madaraka ya kuongoza jimbo la Bukoba na si kwa ajili ya kwenda kuhiji MUGANA pekee bali hata kwenye shughuli za mazishi na hata kusafirisha maiti.

Zaidi ya yote mfano wa haraka mbunge ametoa usafiri kwa timu ya mpira BUKOBA VETERAN kwenda Uganda ili kuiunga mkono timu ya taifa, mbona hiyo hawazungumzi kuwa ni makosa? Yeye anapotoa fedha kwa ajili hiyo si nafasi yake kusimamia kama kilichokodwa ni malori au tax hiyo ni kazi ya waliokabidhiwa kitita.

Unaposisitiza kuwa mbona hajaenda MAKA ili aitwe alhaji nadhani ameona gharama hiyo si sahihi kujinufaisha yeye bali wananchi wake kwasababu kipindi hicho ndicho maeneo kadha ya jimbo yalikumbwa na upepo akatoa msaada wa mabati kwa makanisa ya KYAKAILABWA na KILIMAHEWA pamoja na chakula kwa waliokubwa na upepo ambao ulifikia zaidi ya milioni 5 ambapo kwenda MEKA ni dola zaidi ya 900.

Kama kutoa msaada kanisani ni kosa mbona mabati hayajalalamikiwa?
Mwanafizikia wa kale duniani ALBERT EINSTEIN kutoka ULM WURTTEMBER UJERUMANI, alisema “BINADAMU YEYOTE ANAYESOMA SANA NA AMBAYE HUTUMIA KIDOGO MNO UBONGO WAKE MARA NYINGI HUANGUKIA KATIKA TABIA YA KIVIVU YA KUFIKIRI” Nimesema hivyo kwasababu waliowengi wanaoonekana kupinga ni wale wanaosoma sana na kupenda kuiga pasipokujipatia muda wa kufikiri kwamba majimbo yanatofautiana.

Mbunge kupita kila siku anaenda kuudhuria vikao vya madiwani ni kweli kwamba anatatua matatizo ya wananchi wake kama afanyavo Kagasheki? Ni bora asijitokeze kila siku kmwenye vikao kama unavyopenda aige lakini afanikiwe kuwafikia wananchi mapema na kutatu matatizo yao, lakini kama zilivyo sheria za nchi, vikao vikifanyika ni lazima viwe na maandishi ambayo kulingana na taratibu yatakwenda ngazi moja hadi nyingine katika uongozi, je hayo yanafanyika katika vikao vya madiwani Manispaa ya Bukoba?

Itakumbukwa tangu mwaka 2011 mbunge amekuwa akishiriki na hasa akizungumza kupitia mikutano ya adhara kwa kuzungumzia miradi ya maendeleo ikiwamo suala la kuvunja na kujenga soko kuu jipya la Bukoba, ambapo iko katika ushirikiano wa pamoja, lakini kwakuwa kila kitu kina ngazi yake imekuwa ni kawaida Meya akaratibu baadhi ya masuala lakini ni lazima atoe taarifa kupitia vikao na hata kuwasilisha vielelezo kwa mbunge, ila amekuwa hafanyi hivyo na hilo ndo lalamiko la Kagasheki baada ya kuonekana baadhi ya madiwani nao wakihoji lakini wakiogopa kutokana na ubabe wa meya, wakisubiri Kagasheki aulize ambapo inaonekana wamemtoa kama chambo kwa Meya na wananchi.

Hali hiyo inanionesha na kunikumbusha maneno ya mtunzi maarufu wa kale AGATHA CHRISTIE kupitia kitabu chake cha THE MAN IN THE BROWN SUIT, aliyesema kuwa “NI MAISHA MAGUMU NA AJABU, MWANAUME HAWEZI KUOA MWANAMKE KAMA HANA SURA NZURI NA HAVUTII, NA MWANAMKE HATAMPENDA MWANAUME MWENYE SURA NZURI KUMZIDI NA ANAYEVUTIA”

Kupitia maneno hayo, wananchi watajua nani wanamtaka ili awaongoze na wanampenda wala si vema mtu kujipendekeza katika hilo, wakati mambo muhimu yanafichwa nyumbani mwa familia ya Meya, watu watajuaje? Mbunge akiuliza hilo mnamkandamiza?.

Ya Mungu mpe mungu nay a Kaizali mpeni Kaizali, Balozi HAMIS KAGASHEKI unapigana na wananchi wako ila wanaokusakama wanataka nafasi tu, ila kwasababu hawana jinsi wametafuta namna ya kukuchafua.

Mwanafalsafa SOCRETS wa ITALIA katika miaka ya 500-400 kabla ya Kristo, alisambaza elimu kupitia maandiko akiwataka wananchi kusimama kidete katika maslahi yao, lakini waliokuwa na uchu wa madaraka wakiongozaz wananchi mbumbumbu, baada ya kuona Socret anatoa elimu na wananchi wanapata mwamko, walimlazimisha ajiue kwa kunya sumu mwenyewe, lakini kabla hajainywa alisema “VIONGOZI WENYE TAMAA WAMEAMUA KUUA KICHWA KIMOJA, LAKINI WAMESHINDWA KUJUA KWAMBA NIMEKUFA MIMI ILA ELIMU YANGU IMEJAA TAYARI VICHWANI MWA RAIA, HIVYO WATAENDELEZA MAPAMBANO NA KUJIKOMBOA KUTOKA MIKONONI MWA UBWENYENYE”

Kagasheki hata wakikufitini kisiasa hawa wenye tamaa, naamini ujumbe wako tayari wananchi wameupata na kwasasa wanajua kudai haki na ndo maana baada ya tamko lako kwenye mkutano wa hdahara tarehe 24 november 2012 ulisema soko halijafanyiwa upembuzi yakinifu hivyo halitabomolewa kwa haiwezekani ukajenga sehemu usiojua kiasi cha maji chini ya ardhi.

Ndipo siku moja baadaye ikiwa ni jumapili, kampuni isiyojulikana inayojiita GEOPINIUS INVESTMENY iliyoandikwa kwa MAKERPEN ubavuni mwa gari aina ya FUSO T675 AEJ kutoka Dar es salaam kwa mujibu wa (kandayaziwaleo.blogspot.com) ya huko Bukoba, ilikuja na mashine za kuchimba na kupima kiasi cha maji ndani ya soko kuu, lakini kwa akili uliowapa wananchi wakatambua haki yao walizuia gari hiyo kwani Kesi ya soko bado iko mahaklamani, je anayesema soko lazima livunjwe amepanga na mahakama kwamba lazima ashinde kesi hiyo na mbona anataka kulivunja kabla ya machi ambapo kesi inasikilizwa tena?
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

 
Designed and Bloggerized by | Tryphone Chasama Jr | 0719 625003/0765860437
Proudly powered by BONGO BLOG DESIGNERS
Copyright © 2012. HABARI BONGO - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template