Rais wa Marekani Barack Obama amemshtumu mpinzani wake wa chama cha
Republican, katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa urais wa mwezi Novemba
Mitt Romney, kwa kubagua sehemu kubwa ya raia wa Marekani.
Bwana Romney alinaswa kisiri kwenye ukanda wa video akitoa matamshi ya
kuwadharau baaadhi ya wapiga kura wakati wa hafla ya faragha ya
kuchangisha pesa za kampeni katika chama cha Republican.
Akizungumza kwenye mahojiano na kipindi kimoja cha televisheni nchini
Marekani Obama amesema jambo ambalo amejifunza akiwa rais ni kuwatumikia
wamarekani wote.
Baada ya kuchaguliwa , alisema , atajitahidi kuwahudumia hata wale ambao hawakumpigia kura.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !